Dr Didas Lunyungu akitoa cheti cha kufuzu mafunzo ya Ujasiriamali kwa wajasiriamali waliohudhuria semina iliyofanyika kwenye ukumbi wa Africenter Ilala jijini Dar es Salaam
Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyokuwa yakiendelea kwenye ukumbi wa Africenter Ilala jijini Dar, yanatarajiwa kukamilika leo
Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi wa kampuni ya Mjasiriamali Kwanza inayoendesha semina hizo kubwa hapa nchini Dr Didas Lunyungu amesema kuwa amefanikiwa kutoa vyeti zaidi ya 1000 kwa wajasiriamali waliokuwa wakihudhuria mafunzo kwenye semina hizo baada ya kufaulu kwao vizuri na kuwa tayari kwa kujitengenezea bidhaa majumbani mwao na kuuza kwa wateja ili kujiongezea kipato.
"Tumefanikiwa kutoa vyeti zaidi ya 1000 kwa wajasiriamali walifaulu vizuri mafunzo yao huu ni mwanzo wa harakati zetu kuwafanya watanzania kuondokan ana woga wa ugumu wa maisha kwa kujitengenezea bidhaa ambazo watauza na baadae kujipatia fedha za kuendesha maisha" alisema Didas.
0 COMMENTS:
Post a Comment