WATU zaidi ya 3500 walijitokeza kupokea mafunzo ya Ujasiriamali kutoka kwa Mwalimu mwenye uzoefu na mafanikio makubwa kwenye kufundisha masomo hayo Dr Didas Lunyungu, yaliyofanyika kwa siku nne mfululizo katika ukumbi maaraufu wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar Es Salaam.
Katika mafunzo hayo yaliyohudhuliwa pia na vyombo mabalimbali vya habari nchini, wajasiriamali walijifunza kwa vitendo kutengeneza bidhaa mbalimbali za nyumbani na mashabani, zikiwemo sabuni za kufulia, Batiki, na vitu vingine vingi.
Mmoja ya wajasiriamali waliojitokeza katika semina hiyo Bi Neema Mussa aliuambia mtandao huu kuwa kampuni ya Mjasiriamali kwanza nchini ya Dr Didas ni mkombozi mpya wa maisha ya Watanzania wengi ambayo yako kwenye hali tete kutokana na kukosekana kwa uchumi imara hapa nchini.
"kwa kweli kampuni hii inafanya jambo jema na kubwa sana ambalo linatukomboa wananchi wengi hivi sasa kutoka mdororo wa kiuchumi tulionao kutokana na mafundisho bora ya kutengeneza bidhaa tunayaopata tukiwa kwenye semina" alisema.
Akiendelea zaidi Bi Neema alitoa wito kwa serikali kuipa nguvu kampuni hii ili iweze kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao kwa hakika wan awakati mgumu kimaisha na kuwakomboa kutoka shida nyingi za ukosefu wa fedha jambo linaweza kuharakisha maendeleo miongoni mwao
Mmoja wa maelfu ya wajasiriamali, akifanya maohjiano na mtangazaji wa runinga ya Taifa TBC, wakati wa semina kubwa iliyofanyika ndani ya DAR LIVE Mbagala jijini Dar.
Maelfu ya wakazi wa jiji na wengine kutoka mikoa mbalimbali nchini wakitoka ndani ya ukumbi wa Dar Live mara baada ya kumalizika kwa semina ya ujasiriamali iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Mjasiriamalikwanza Dr Didas Lunyungu mwishoni mwa wiki iliyopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment