MAHOJIANO NA TBC 1

Mkurugenzi wa kampuni ya Mjasiriamali Kwanza Dr Didas Lunyungu akifanya Mahojiano na mtangazaji wa Runinga ya TBC 1 Eddie Ganzel.

DARASA LILIWA MAKINI

Wajasiriamali zaidi ya 1200 waliojitokeza kwenye semina inayofanyika ndani ya ukumbi wa Sunset ulio Mbezi Beach wakiwa makini kusikiliza mafunzo hayo.

MAJADILIANO

Mkurugenzi wa kampuni ya Mjasiriamalikwanza Dr Didas Lunyungu akiwa amepozi akisikiliza kwa makini majadilinoya wajasiriamali baada ya somo husika.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, June 17, 2013

MATUKIO SIKU YA KWANZA SEMINA SUNSET HALL MBEZI BEACH

Mwalimu na Mkurugenzi wa Kampuni ya mjasiriamalikwanza Dr Didas Lunyungu akitoa somo kwa wajasiriamali zaidi 1200 kwenye ukumbiwa Sunset uliopo Mbezi Beach makonde jijini Dar.


Kundi la wajasiriamali zaidi ya 1200 waliojitokeza kwenye ukumbi wa Sunset  uliopo mbezi beach makonde jijini dar
Darasa linaendelea kwa siku tatu, hapa ilikuwa ni wakati wa  somo la  kutengeza sabuni ya maji

Friday, May 3, 2013

MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MAILI MOJA


 Muasisi wa mafunzo ya ujasiriamali nchini Dr Didas Lunyungu, akitoa somo kwa Wajasiriamali zaidi ya 800 waliojitokeza  kwenye mfululizo wa semina za siku tatu kwenye ukumbiwa Country Side uliopo kibaha Maili Moja  makoani Pwani.
 Hapa ni Mwalimu wa somo la Batiki Mama Gaitan (kushoto) akiwa katika hatua za awali za kufunga umbo la nyota tayari kwa somo la  utengenezaji wa Batika ambapo wajasiriamali zaidi ya 800 walijifnza somo hilo.
 Meneja wa Kampuni ya Mjasiriamali kwanza  ambaye pia ni Mwalimu akifundisha somo la  usindikaji wa  Maziwa  kwenye  ukumbi wa Country Side Kibaha Maili Moja mbele ya wajasiriamali zaidi ya 800.
 Kundi kubwa la Wajasiriamali  wakipeana Mikono kufurahia moja ya Mafunzo kutoka kwa walimu wa kampuni ya Mjasiriamali kwanza.
Mwali wa somo la Batiki, Mama Gaitan akioa maelekezo kwa wajasiriamali namna ya kutengeza Batiki ikiwa na umbo la Nyota.

Wednesday, November 28, 2012

SEMINA KUBWA YA UJASIRIAMALI YATIKISA DAR

 Wajasiriamali kutoka kikundi mojawapo kati ya vingi vilivyokuwepo kwenye semina kubwa ya iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Afri Center na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 1200 wengi wakiwa kutoka nje ya jiji la Dar .
 Hapa Wajasiriamali wakijifunza kwa vitendo kutengeneza dawa ya usafi
 Masomo yanaendelea
 Hapa wajasiriamali wakijipogeza baada ya kufanikiwa kutengeneza moja ya bidhaa na mwalimu Saravai mwenye koti kuwafahamisha kuwa wamefaulu zoezi lao
 Kazi na dawa Dj Mdoe akiwa kwenye mashine kutoa burudani kwa wajasiriamali tayari kwa masomo mengine  ndani ya ukumbi wa AfriCenter Ilala jijini Dar.




Friday, September 14, 2012

WAJASIRIMALI WALIOFUZU WAPEWA VYETI

 Dr Didas Lunyungu  akitoa cheti  cha kufuzu mafunzo ya Ujasiriamali kwa  wajasiriamali waliohudhuria semina iliyofanyika kwenye ukumbi wa Africenter Ilala jijini Dar es Salaam

 
Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyokuwa  yakiendelea kwenye ukumbi wa Africenter Ilala jijini Dar, yanatarajiwa kukamilika  leo 
Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi wa kampuni ya Mjasiriamali Kwanza inayoendesha  semina hizo kubwa hapa nchini Dr Didas Lunyungu amesema kuwa amefanikiwa kutoa vyeti zaidi ya 1000 kwa wajasiriamali waliokuwa wakihudhuria mafunzo kwenye semina hizo baada ya kufaulu kwao vizuri na kuwa tayari kwa  kujitengenezea bidhaa majumbani mwao na kuuza kwa wateja ili kujiongezea kipato.

"Tumefanikiwa kutoa vyeti zaidi ya 1000 kwa wajasiriamali walifaulu vizuri mafunzo yao huu ni mwanzo wa harakati zetu kuwafanya watanzania  kuondokan ana woga wa ugumu wa maisha kwa kujitengenezea bidhaa ambazo watauza na baadae kujipatia fedha za kuendesha maisha"  alisema Didas.

Monday, September 3, 2012

3500 WAHUDHURIA MAFUNZO DAR LIVE

WATU zaidi ya 3500 walijitokeza kupokea mafunzo ya Ujasiriamali kutoka kwa Mwalimu mwenye  uzoefu na mafanikio makubwa  kwenye kufundisha  masomo hayo Dr Didas Lunyungu, yaliyofanyika kwa siku nne mfululizo katika ukumbi maaraufu wa  Dar Live  uliopo Mbagala  jijini Dar Es Salaam.

Katika mafunzo hayo yaliyohudhuliwa  pia  na vyombo  mabalimbali vya habari nchini, wajasiriamali walijifunza kwa  vitendo kutengeneza  bidhaa mbalimbali za nyumbani na mashabani, zikiwemo sabuni za  kufulia, Batiki, na  vitu vingine  vingi.

Mmoja  ya wajasiriamali waliojitokeza katika  semina hiyo Bi Neema  Mussa aliuambia  mtandao huu kuwa kampuni ya  Mjasiriamali kwanza nchini ya Dr Didas  ni mkombozi mpya wa maisha ya Watanzania  wengi  ambayo yako kwenye hali tete  kutokana na  kukosekana kwa  uchumi imara hapa nchini.

"kwa  kweli kampuni hii  inafanya jambo jema  na kubwa  sana  ambalo linatukomboa wananchi wengi hivi sasa  kutoka  mdororo wa  kiuchumi tulionao kutokana na mafundisho bora  ya kutengeneza bidhaa  tunayaopata  tukiwa kwenye semina"  alisema. 

Akiendelea  zaidi  Bi Neema alitoa wito kwa serikali kuipa  nguvu kampuni hii  ili iweze kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao  kwa hakika  wan awakati mgumu kimaisha  na kuwakomboa  kutoka  shida nyingi za  ukosefu wa fedha jambo linaweza kuharakisha  maendeleo miongoni mwao
Mmoja wa maelfu ya wajasiriamali, akifanya  maohjiano na mtangazaji wa  runinga ya Taifa TBC, wakati wa  semina  kubwa  iliyofanyika ndani ya DAR LIVE Mbagala jijini  Dar.
Maelfu ya wakazi wa jiji na wengine  kutoka  mikoa mbalimbali nchini wakitoka ndani ya ukumbi wa Dar Live  mara baada ya kumalizika kwa semina  ya ujasiriamali iliyokuwa  ikiongozwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Mjasiriamalikwanza Dr Didas Lunyungu mwishoni mwa  wiki iliyopita. 

Wednesday, June 20, 2012

MMESIKIA JAMANI..

 Dk Didas akitoa maelezo kwa wajasiriamali waliojitokeza kumsikiliza
 Afisa masoko wa kampuni ya Mjasiriamali Kwanza  ndugu Isaya (kushoto) akitoa moja  ya malighafi za kutengenezea sabuni kwa mjasiriamali Veronicka wa Kimara Dar es Salaam.
Wajasiriamali wakijadiri jambo baada ya kupata mafunzo kutoka kwa  Dk Didas Lunyungu.

MAFUNZO KWA VITENDO

 Dk  Didas akitoa maelezo kwa vitendo jinsi ya  kutengeneza  sabuni ya maji  kwa  kuchanganya aina  mbalimbali za malighafi wakati wa semina hiyo  ndani ya ukumbi wa Afri Center Ilala. Dar es Salaam.
                         Hapa Dk Didas akichanganya  malighafi kwenye ndoo ndogo ya plastiki
Hapa akitoa maelezo mafupi baada ya kukamilika kwa zoezi hilo  na hatimaye sabuni ya maji kupatikana